BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI,ZILIZOBADILISHWA LEBO ZAKAMATWA KWENYE MADUKA SHINYANGA MJINI


Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga ikishirikiana na wakaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS imefanikiwa kukamata bidhaa zilizoisha muda wa zikiendelea kuuzwa katika maduka makubwa maarufu kama Supermarket mjini Shinyanga hali ambayo ni hatari kwa afya za watumiaji wa bidhaa hizo.


Bidhaa hizo zimekamatwa jana kutokana na msako katika maduka mbalimbali Mjini Shinyanga na kukamata shehena ya bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula na vipodozi ambazo zimeisha muda wa kutumika vikiendelea kuuzwa madukani.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo,Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga amesema licha bidhaa nyingi madukani kuwa zimeisha muda wa kutumika pia wamebaini kuna udanganyifu mkubwa wa kubadilisha lebo za muda wa matumizi katika bidhaa mbalimbali ili ziendelee kuuzwa sokoni.

Naye Mkaguzi wa kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS Helen Andrew amesema operesheni hiyo sasa ni endelevu kwa mikoa yote.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia bidhaa ndani ya duka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527