BARAZA LA WAZEE LA CHADEMA LABARIKI CHAMA HICHO KUJITOA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 8, 2019

BARAZA LA WAZEE LA CHADEMA LABARIKI CHAMA HICHO KUJITOA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

  Malunde       Friday, November 8, 2019

Baraza la wazee la  Chadema limebariki uamuzi wa chama hicho kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 8, 2019 mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma Issa amesema ilikuwa lazima chama hicho kijitoe kutokana na kutengenezewa mazingira ya kufanya hivyo.

Issa amekwenda mbali zaidi na kuwataka wanachama wao kote nchini kutotoa ushirikiano kwa viongozi watakaoteuliwa kushika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

“Hatuna sababu ya kushirikiana nao kwa kuwa wameteuliwa na sisi tunahitaji viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kidemokrasia,” amesema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post