WAZIRI JAFO AWATAKA WAKUU WA SHULE KUTOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU WA MITIHANI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 1, 2019

WAZIRI JAFO AWATAKA WAKUU WA SHULE KUTOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU WA MITIHANI

  Malunde       Tuesday, October 1, 2019
Na  Faustine Gimu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) SELEMANI JAFO  amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.


Waziri Jafo ametoa agizo hilo  jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara.

Amesema wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.

Akizungumzia suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha), REHEMA RAMOLE ameipongeza serikali kwa uboreshaji wa miundombinu jambo ambalo limepunguza msongamano wa wanafunzi darasani.

Kauli mbiu ya mkutano huo inasema Uwajibikaji na Usimamizi makini wa Rasilimali katika elimu ndio Msingi wa Elimu Bora.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post