Picha : JESHI LA POLISI SHINYANGA LATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WATU WALEMAVU | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 8, 2019

Picha : JESHI LA POLISI SHINYANGA LATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WATU WALEMAVU

  Malunde       Tuesday, October 8, 2019

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog

Ukosefu wa elimu ya Usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga umetajwa kusababisha vifo kwa watu wenye ulemavu kutokana na kugongwa na magari ambapo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita jumla ya walemavu wanne wamepoteza maisha hali ambayo imelilazimu jeshi la polisi mkoani humo kuandaa mafunzo maalumu kwa ajili ya kundi hilo.Hayo yamebainishwa leo mjini Shinyanga na mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu mkoa wa Shinyanga, Richard Mpongo katika mafunzo maalumu kwao na kusema kuwa kundi la walemavu limesahaulika kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa ikisababisha wengi wao kugongwa na magari wakati wakivuka barabara.

Amesema walemavu wanapata changamoto mbalimbali pindi wanapotumia barabara kutokana baadhi ya madereva kutozingatia matumizi sahihi ya barabara jambo ambalo linasababisha kundi hilo kuendelea kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

Awali akimkaribisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga, Anthony Gwandu amesema mafunzo hayo yamejumuisha walemavu zaidi 30 wa aina mbalimbali na mafunzo hayo yatawafikia walemavu wote katika mkoa wa Shinyanga.

“Jeshi la polisi tunashirikiana na wataalamu mbalimbali wa lugha za alama watahakikisha walemavu wa kuona na kusikia wanapata elimu hiyo muhimu ili kutokomeza ajali za barabarani na kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima",alisema Gwandu.


Akifungua mafunzo hayo ya siku moja, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesema Jeshi la polisi limelazimika kutoa mafunzo hayo kwa walemavu baada ya kubaini kusahaulika kwa muda mrefu huku Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Gwandu akiwasisitiza matumizi sahihi ya alama za barabarani.


Ameongeza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua kali Madereva wote watakaobainika kutozingatia matumizi sahihi ya alama za barabara ikiwemo katika maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu ambavyo vinatumiwa na watu mbalimbali ikiwemo wenye ulemavu.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao akizungumza jinsi walivyoamua kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mbalimbali ili kuepukana na ajali za barabarani.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Shinyanga (RTO), Athony Gwandu akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mbalimbali mkoani Shinyanga.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga (RTO), Athony Gwandu akimsikiliza Yohana Isabu mwenye ulemavu wa macho namna ya kuwasaidia walemavu kukabiliana na ajali za barabarani.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO), Emmanuel Palangyo akitoa elimu ya usalama barabarani kwa walemavu ili kuepukana na ajali hasa kwenye maeneo ya vivuko.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO),Emmanuel Palangyo akiendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu ili kuepukana na ajali.

Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Mafunzo ya usalama barabarani yakiendelea.


Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo
(kulia) akipongeza utolewaji wa elimu hiyo ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu.

Yohana Isabu ambaye ni mlemavu wa macho, akishukuru elimu hiyo ya usalama barabarani na kuomba wadau wajitokeze kusaidia ugawaji wa fimbo nyeupe hasa kwa walemavu wa macho ili ziwasaidie muongozo wa kutembea na kuepukana na ajali.

Elizabeth Mathayo akishukuru utolewaji wa elimu hiyo ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu ambayo itakuwa msaada wao mkubwa kuondokana na ajali za barabarani zisizo za lazima.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao akipiga picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi hilo kikosi cha usalama barabarani pamoja na watu wenye ulemavu mara baada ya kuwapatia elimu ya usalama barabarani.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post