ALLIANCE FC YATUA KENYA KUWEKA KAMBI KUWAVAA YANGA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 8, 2019

ALLIANCE FC YATUA KENYA KUWEKA KAMBI KUWAVAA YANGA

  Malunde       Tuesday, October 8, 2019
Timu ya Wachezaji wa Alliance FC wakiwa pamoja na benchi la ufundi na Wafanyakazi wa Access Bank
Jackson Luka Mwafulango Afisa Habari wa Alliance FC akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Alliance FC Yusuph Budodi na Meneja wa Access Bank Mwanza Emmanuel Venance wakizungumza na Wanahabari kuhusu timu ya Alliance FC kuweka kambi Nairobi Kenya.
Meneja wa Access Bank Emmanuel Venance akizungumza na  waandishi wa habari Ziara ya Alliance FC Kenya


Timu ya Soka ya Alliance FC ya Mwanza imeondoka leo kwenda Nairobi Nchini Kwenye kuweka kambi kujiandaa na mechi ya Yanga itakayochezewa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza tarehe 20 Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa kuiaga timu hiyo,  Meneja wa Benki ya Access tawi la Mwanza Emmanuel Venance amesema wana faraja kubwa kuwa mmoja wa wadhamini wa timu hiyo kutokana na inavyojituma uwanjani. 

Amesema kama Taasisi ya Kifedha hapa Nchini wataendelea kuunga mkono juhudi za Timu hiyo wakishirikiana na wadhamini wengine kuhakikisha timu ya Alliance FC inakuwa Moja Kati ya timu tishio hapa Nchini.

Awali akimkaribisha Meneja wa Access Bank, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Alliance FC Yusuph Budodi ameishukuru Access Bank  pamoja wadhamini wengine wanaoidhamini Timu hiyo, na kuwaahidi kuendelea Kufanya kazi nzuri ili kupata pointi za Kutosha kwenye michuano ya ligi Kuu na mashindano mengine kwa Mujibu wa TFF.

Pamoja na Access Bank, wapo wadhamini wengine Kama Alliance Schools, Emirates Alluminium Profile na Mwanza Pure Drinking Water. Alliance FC wameondoka Leo kwenda Nairobi Kenya, kujiandaa na mechi nguma ya ligi didhi ya  timu ya Wananchi Yanga.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post