MBWANA SAMATTA AFUNGA NDOA


Samatta na mkewe baada ya kufunga ndoa

Ni likizo ya kimataifa na wachezaji wenzake wengi wapo katika zamu ya kimataifa lakini nahodha wa timu ya Taifa Stars na KRK Genk Mbwana Samatta alikuwa na mipango mingine kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.

Mshambuliaji huyo matata alitumia wakati wake mzuri wa likizo hiyo siku ya Alhamis kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Neima Mgange.

Sherehe ya harusi yake iliofanyika katika kijiji cha kijichi mjini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars akiwemo Himid Mao na Thomas Ulimwengu kulingaa na gazeti hilo.

Ilikuwa sherehe ya kufana miongoni mwa watu wa familia ya Mgange walipokutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Maelezo kuhusu uhusiano wa Mbwana na Neima yalikuwa ya siri kubwa na ni watu wa familia zote mbili pekee waliokuwa wakielewa kilichokuwa kikiendelea hadi siku ya Alhamisi.

Mshambuliaji huyo hakushirikishwa katika mechi ya kimataifa ambayo Taifa Stars inacheza dhidi ya Uganda wikendi hii.

Alikuwa akiugua jeraha lakini akashirikishwa katika kikosi cha timu ya Genk kilichopoteza 6-2 dhidi ya klabu ya Salzbourg kutoka Austria katika michuano ya kombe la mataifa bingwa Ulaya.

Pia aliisaidia Tanzania katika michuano ya kimakundi ya kufuzu kwa kombe la dunia Qatar 2022.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527