RWANDA YAZINDUA BANDARI KAVU YENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 35


Rais Paul Kagame wa Rwanda amezindua bandari kavu ya ugavi mjini Kigali, ikayotaifanya Rwanda iwe kitovu cha usafirishaji wa mizigo cha kanda hiyo.

Bandari hiyo yenye ukubwa wa mita elfu 2.5 za mraba, pia itatumiwa na kituo cha uvumbuzi wa Yiwu cha Jukwaa la biashara ya kielektroniki ya kimataifa la Alibaba (eWTP).

Kampuni kubwa zaidi ya China ya biashara ya kielektroniki ya Alibaba na kampuni ya uendeshaji wa bandari ya Dubai Ports World, zinalenga kujenga ghala hilo kuwa ghala kuu la bidhaa za China katika eneo la Afrika Mashariki na kuvumbua mfumo mpya wa kuingiza na kuuza bidhaa nje.

Habari zinasema, bandari hiyo inayogharimu dola za kimarekani milioni 35 ina yadi ya vyombo vya usafirishaji yenye ukubwa wa mita elfu 12 za mraba, na kituo cha ghala chenye ukubwa wa mita elfu 19.6 za mraba. 

Uwezo wake wa kuhifadhi mizigo utafikia tani laki 6.4 kwa mwaka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527