PROFESA TIBAIJUKA KUREJESHA SHILINGI 1.6 BILIONI ZA MGAO WA RUGEMARILA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 2, 2019

PROFESA TIBAIJUKA KUREJESHA SHILINGI 1.6 BILIONI ZA MGAO WA RUGEMARILA

  Malunde       Wednesday, October 2, 2019
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea  kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.


Profesa Tibaijuka amesema hayo kupitia Kituo cha televisheni cha Azam TV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha  fedha hizo walizopokea ili kumsaidia  mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa,  Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

==>>Msikilize hapo chini


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post