RC CHALAMILA SASA KUWACHAPA VIBOKO WALE HAWAJAOA AU KUOLEWA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema kwa sasa atakuja na mpango wa kuwachalaza bakora wanawake na wanaume mkoani kwake, ambao hawajaoa au kuolewa na kueleza akishamaliza kuwachapa, atawaagiza waende wakatafute wapenzi wao wa kufunga nao ndoa.

Chalamila ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya, ambapo amesema njia ya kutumia bakora ni miongoni mwa njia ambazo zinasaidia sana kwenye kuhamasisha jambo.

"Siku hizi tunatumia bakora katika kila jambo, tukikukuta umekaa nyumbani na huolewi ni bakora tu nenda katafute mume na ukiwa umekaa nyumbani huoi ni bakora tu nenda katafute mke, kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe'' amesema Chalamila.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527