CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA CHAPOKEA MASHINE YA KISASA YA KUPIMA UBORA WA CHUJIO ZA MAGARI(FILTERS) | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 23, 2019

CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA CHAPOKEA MASHINE YA KISASA YA KUPIMA UBORA WA CHUJIO ZA MAGARI(FILTERS)

  Malunde       Wednesday, October 23, 2019

Afisa Tawala wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,Anaclet Mushashu(wa pili kulia) Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela(NM-AIST),Profesa Anthony Mshandeti(wa pili kushoto),Mkurugenzi wa taasisi Kotra,Hong Kyun Lee na Meneja Biashara wa ART+,Insoo Chang(kulia) wakizindua matumizi Mashine ya kupima ubora wa Chujio za magari(Filters) yenye thamani ya dola 100,000 katika Chuo Kikuu cha MN-AIST. 
***

Taasisi ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandela(NM-AIST) imenufaika na msaada wa mashine yenye uwezo wa kupima ubora wa Chujio za magari zinazotengenezwa hapa nchini na nje ya nchi ili kutunza afya za watu

Mradi huo unatekelezwa na Kituo cha Umahiri cha Wise-Future ili kutoa fursa kwa wanafunzi kunufaika na ufadhili wa elimu ya juu katika eneo la utaalamu maji na nishati.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Anthony Mshandeti akizungumza wakati wa kuzindua mashine hiyo yenye thamani ya dola laki moja iliyotolewa na shirika la Aerosol Research and Technology Plus(ART+) ya Korea amesema itatoa mchango muhimu katika kutunza mazingira.

“Wanafunzi wetu wanaofanya tafiti mbalimbali na wenye ndoto za baadaye kufungua viwanda vya kuzalisha chujio za magari na mitambo watanufaika na uwepo wa mashine hii ambayo itakua ikitoa majibu ya ubora wa chujio zao ndani ya muda mfupi,”amesema Mshandeti

Meneja Biashara wa kimataifa wa ART+,Insoo Chang amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la Afya duniani(WHO) za mwaka 2018 watu wapatao milioni moja kila mwaka barani Afrika wanapoteza maisha kutokana na uchafuzi wa hewa.

“Mabadiliko ya Tabia Nchi  yamekua ni mambo yanayozungumzwa dunia nzima katika miaka ya hivi karibuni pia yanaathari au kutoa mchango katika hali ya hewa ya hapa Tanzania kwani mnaweza kushudia nyakati za mvua hazinyeshi au zinanyesha wakati wa kiangazi ni mambo ambayo tunapaswa kuyapa umakini katika kuyashughulikia,”amesema Chang
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post