MBUNGE WA JIMBO LA NDANDA CECIL MWAMBE AJITOSA KUMRITHI MBOWE UENYEKITI CHADEMA


Mbunge wa Jimbo la Ndanda (CHADEMA) ambaye ni  Mjumbe wa Kamati kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Mh Cecil Mwambe ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa, akiahidi kuleta mabadiliko kadhaa katika chama hicho.


Chadema imepanga kufanya uchaguzi wake mkuu Desemba 18, mwaka huu.

Bado haijafahamika kama  Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe atagombea  tena au  hatagombea.

Uongozi wa Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ulimalizika Septemba 14 na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa siku saba zinazomalizika leo saa 9.30 alasiri wawe wamewasilisha maelezo kwa nini hawajafanya uchaguzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post