Picha : AGAPE YAKUTANA NA MADIWANI KUJADILI NAMNA YA KUTOKOMEZA UKATILI KWENYE MASOKO SHINYANGA



Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, limefanya kikao na madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kujadili namna ya kutokomeza ukatili masokoni.


Kikao hicho kimefanyika leo Oktoba 30, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Katemi Shinyanga mjini, na kuhudhuriwa pia na viongozi wa masoko sita ya Shinyanga mjini, pamoja na maofisa Maendeleo na ustawi wa jamii Manispaa na mkoa wa Shinyanga.

Akifungua  kikao hicho, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Agape John Myola, amesema wamefanya kikao hicho na waheshimiwa madiwani, ambao ndiyo watunga sheria za manispaa ya Shinyanga, ili kuona namna watakavyoshirikiana kwa pamoja kutokomeza ukatili kwenye masoko.

Amesema katika utekelezaji wa mradi wao wa “Mpe Riziki si Matusi” ambao unafadhiliwa na Shirika la kimataifa la UN WOMEN kupitia shirika la Equality for Growth (EFG), wamedhamilia kutokomeza ukatili kwenye masoko sita ya manispaa ya Shinyanga dhidi ya wanawake na wasichana, ambayo ni Kambarage, Soko kuu, Nguzo nane, Ngokolo, Majengo Mapya, na Ibinzamata.

“Tumefanya kikao hiki na madiwani wa manispaa ya Shinyanga ambao ndiyo watunga sheria za manispaa, ili kujadiliana kwa pamoja kuona namna tukavyoshirikiana kutokomeza ukatili wa wanawake na wasichana kwenye masoko yetu ya manispaa ya Shinyanga, ikiwamo kuondoa lugha chafu za matusi, dhuluma, kushikwa maumbile yao, kutakwa kimapenzi kwa nguvu pamoja na vipigo,” amesema Myola.

Naye Afisa mradi wa kutokomeza ukatili masokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ Helena Daudi, amesema Mradi huo umeanza kutekelezwa tangu Novemba mwaka 2018 ambao unakoma mwaka huu Oktoba 2019, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza ukatili huo kwa kiwango kikubwa.

Amesema awali kabla ya kuanza mradi huo, walifanya utafiti na kukutana na vitendo vingi  vya ukatili kwenye masoko ya manispaa ya Shinyanga, na kuamua kuanza kuutekeleza ili kupunguza ukatili kwenye maeneo hayo ya Soko na kuwa mahali salama pa kufanyia biashara, na siyo vijiwe vya udhalilishaji wanawake.

Aidha Mratibu wa dawati la kuzuia ukatili kwenye masoko ya manispaa ya Shinyanga Angel Mwaipopo, amekiri ukatili huo kwa sasa umepungua kwa kiwango kikubwa tofauti na hapo awali, ambapo masoko yao yalikuwa na udhalilishaji mkubwa wa kijinsia.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii mkoani Shinyanga Lyidia Kwesigabo, ametaja matukio ya ukatili kwa mkoa mzima, kuwa kuanzia mwaka wa fedha Julai 2018-Juni 2019, kuwa yametokea matukio ya ukatili 2,588 wanawake wakiwa 1,940 na wanaume 648.

Nao madiwani hao walikiri kuwepo na ukatili kwenye masoko, ambapo kwenye kikao hicho wameahidi kushirikiana na Shirika hilo la Agape ili kutokomeza ukatili, pamoja na kuhamasisha kutengwa kwa bajeti kwenye halmashauri ili kusaidia mpango mkakati wa taifa wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA uweze kufanikiwa kwa asilimia 100.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akizungumza kwenye mkutano na madiwani na manispaa ya Shinyanga namna ya kushirikiana kwa pamoja kutokomeza ukatili sokoni ikiwamo na kutunga Sheria ndogo za kutoa adhabu kwa watu ambao wanafanya ukatili huo.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akielezea mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa Mpe Riziki Si Matusi namna unavyo fanya kazi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko ya Shinyanga mjini.

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili kwenye masoko "Mpe Riziki si Matusi" Helena Daudi akielezea namna walivyopambana kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko ya Shinyanga Mjini.

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili kwenye masoko "Mpe Riziki si Matusi" Helena Daudi akielezea namna walivyopambana kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko ya Shinyanga Mjini.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akielezea namna walivyofanya utafiti wa awali na kubaini kuwepo na ukatili wa wanawake kwenye masoko na kuamua kuanzisha mradi wa kupambana na ukatili huo.

Mratibu wa dawati la kuzuia ukatili kwenye masoko ya manispaa ya Shinyanga Angel Mwaipopo akielezea namna mradi wa Shirika la Agape ulivyosaidia kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana sokoni.

Afisa ustawi wa jamii mkoani Shinyanga Lydia Kwesigabo, akielezea hali ya ukatili kwa mkoa mzima ambapo wanawake ndio wanaongoza kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Madiwani wakiwa kwenye kikao.

Madiwani wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Lubaga manispaa ya Shinyanga Obed Jilala akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga Paulo Machela akichangia mada kwenye kikao.Diwani wa Kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga Hassani Mwendapole akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga Wiliamu Shayo akichangia mada kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya vikundi kujadili namna ya kutokomeza ukatili kwenye masoko ya Shinyanga Mjini dhidi ya wanawake na wasichana.

ajumbe wakiendelea na kazi ya vikundi.

Wajumbe wakiendelea na kazi ya vikundi.

Wajumbe wakiwasilisha kazi ya vikundi, namna walivyojadili jinsi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko sita ya Shinyanga Mjini.

Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.

Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.

Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527