KUTANA NA BIBI MWENYE UMRI WA MIAKA 102 ANAYEKWENDA GYM

Bibi mwenye umri wa miaka 102 Ider Wheeler, ameeleza siri ya kufikia umri huo na kuonekana mwenye nguvu na afya njema ni kwenda Gym kubeba chuma, mazoezi ambayo anayafanya mara tatu kwa wiki.

Bibi huyo ambaye ametimiza umri huo wiki iliyopita, amesema alianza Gym mwaka 1970, na hajawahi kukosa kuacha kwenda kufanya mazoezi hayo hata katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake, bado alienda Gym na mjukuu wake aitwaye Shirley Rodgers.

Aidha kwa upande wa mjukuu wake huyo amesema, anampa hongera bibi yake huyo kwa kuwa na afya njema hadi sasa, kujipikia chakula mwenyewe, kufanya shughuli za kimwili licha ya kufikia umri huo na kusoma habari kila siku.

Pia mjukuu wake huyo amendelea kusema "Dhahiri kabisa anani-inspire sana na kiukweli ananishangaza, najivunia kuwa na yeye kwa kuwa na umri wa miaka 102 ila bado anafanya kazi" amesema Shirley Rodgers.
Source By Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527