HALMASHAURI YA BUKOBA KUANZISHA KLABU ZA LISHE SHULENI


Afisa lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Desdery Karugaba 

Na Lydia Lugakila- Malunde 1 blog
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa kushirikiana na wadau wa lishe wameweka mkakati wa kuanzisha klabu za lishe katika shule za msingi na sekondari ili kutoa elimu hasa kwa kundi la vijana balehe kutokana na kundi hilo kuwa mahitaji makubwa ya ki lishe.

Hayo yamebainshwa Oktoba 8, 2019 na Afisa lishe wa halmashauri hiyo,Desdery Karugaba wakati wa kikao cha kamati ya lishe kwa kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

Afisa huyo amesema halmashauri hiyo imefanikiwa katika mpango wa lishe kwa makundi ya watoto wachanga,wajawazito isipokuwa kundi ambalo limesahaulika ni vijana balehe ambalo ni kundi muhimu hivyo wamepanga mikakati ya kuanzisha klabu za lishe katika shule za msingi na sekondari.

Amesema vijana balehe (wenye umri wa miaka 9 hadi 20) ni kundi ambalo lina mahitaji makubwa ya ki lishe kwa sababu ukuaji wake huenda kwa kasi na kusababisha mahitaji ya ki lishe kuongezeka hivyo hilo kundi ni lazima lipatiwe elimu ya kutosha ya ki lishe ili kujua ni vyakula gani vinahitajika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527