DC KOROGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA KIKOSI KAZI CHA KURATIBU NA KUSIMAMIA MIRADI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MKOPO WA BENKI YA DUNIA



MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akisisitiza jambo wakati wa mamzungumzo hayo

 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa wa Kujenga Uwezo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Debora Mkwemwa wakati wa mazungumzo hayo


MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa amekutana na kufanya mazungumzo na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwake, Afisa wa Kujenga Uwezo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Debora Mkwemwa alisema kwamba wamefika wilayani humo kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.

Alisema ufuatiliaji huo ni miradi ya ujenzi wa barabara tatu,ujenzi  wa soko ambao tayari umekwisha na stendi kubwa ya mabasi Korogwe  ambayo imekamilika na inatumika kwa sasa hivyo kazi wanayoifanya ni kutaka kuangalia je wana Korogwe kupitia halmashauri na viongozi wanaipokeaji hiyo miradi na wanaisimamia vipi ili waweze kuwahudumia wananchi muda mrefu.

Alisema kwamba pia watawashauri namna ya kuisimami miradi hiyo ikiwemo pia kushauriana kuhusu miradi watakayoipendekeza kwa ajili ya siku zijazo baada ya kukamilika miradi ambayo walioichagua wenyewe huku akieleza wakipata nafasi watapata miradi mingine inayoanza 2020-2021.

Afisa huyo alisema kwamba watashauriana nao kuhusua na miradi watakaokuwa wameichagua ili iweze kuwa miradi rafiki ya kutoa huduma na pia kuwanufaisha wana Korogwe.

Awali akizungumza baada ya mazungumzo hayo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kwamba kama kuna hitaji matokeo ya haraka sana inapaswa wawe wanaweka kwenye jamii ambayo itakuwa inanufaika zaidi

Alisema kwamba amelichukua suala hilo na atakwenda kulifanyia kazi hasa kwaHalmashauri watu wa mipango na wachumi ambao ndio wanaibuni hiyo miradi huku akiwashukuru wao kutaka kushirikiana na viongozi hao ili fedha za miradi zisirudi na yeye kama DC ametambua kwamba  huo ni uzalendo mkubwa kwani kufuatilia jambo ndio mambo yanakwenda hivyo aliwashukuru sana kwa kuwa wamefanya shirikishi hivyo kwa pamoja tutatoka na kitu kimoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527