ALIYELAWITI WATOTO AUAWA KWA KUCHOMWA KISU CHA GEREZANI

Mwanamme Muingereza aliyekuwa akitumikia kifungo gerezani kwa makosa kadhaa ya uhalifu wa kingono dhidi ya watoto wa Malasia amepatikana akiwa amedungwa kisu hadi kufa gerezani.

Richard Huckle, mwenye umri wa miaka 33, kutoka eneo la Ashford, Kent, nchini Uingereza aliwalawiti watoto hadi 200

Mnamo mwaka 2016, alihukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani baada ya kukiri makosa 71 ya ubakaji wa watoto waliokuwa na umri wa miaka kati ya sita na 12 kati ya mwaka 2006 na 2014.

Inafahamika kuwa alishambuliwa siku ya Jumapili alipokuwa katika mahabusu ya gereza la Full Sutton karibu na York, na kisu kinachotumiwa jikoni.

Polisi waliitwa majira ya saa sita usiku na kuanza uchunguzi kuhusina na kifo hicho ambacho wanakishuku.

Katika kesi dhidi ya Huckle mwaka 2016 wapelelezi waliochunguza kompyuta yake walibaini zaidi ya picha na video zaidi ya 20,000 za aibu za matukio yake ya ulawiti wa watoto.

Alizishirikisha kwa walawiti wengine kote duniani kupitia wavuti wa siri uliofahamika kama wavuti wa giza.
Huckle, ambaye alifanyakazi kama mpigapicha wa kujitegemea , alijaribu kutumia unyanyasaji huo wa kingono kwa kuuza picha hizo . Alikuwa akikusanya picha za vitendo hivyo wakati alipokamatwa mnamo mwaka 2014.

Katika mwisho wa kesi yake , Judge Peter Rook alisema kuwa hukumu ya Huckle inaonyesha " kero la umma " kuhusu "kampeni yake ya ubakaji ".

Alisema "Ni nadra sana kwa jaji kumuhukumu mtu mmoja kwa makosa ya ubakaji kwa kiwango hiki ."
Wakazi wakiandamana kupinga mpango wa kupanua gereza la Full Sutton

Huckle alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataiofa wa Gatwick Airport nchini Uingereza na maafisa wa kukabiliana na uhalifu mwezi Disemba 2014, baada ya kupewa taarifa na maafisa wa Australia.

Alijitambulisha kama mkristo na kwamba alitembelea Malaysia kwa mara ya kwanza kama mwalimu alipokuwa na umri wa miaka 18 au 19.

Baadae alikuwa akiwasaidia watoto kukuza vibaji vyao huku akifanya kazi ya kujitolea.

Katika jumbe zake za mtandao, Huckle alituma ujumbe wa mzaha uliosema : "Watoto maskini ni rahisi sana kutongoza kuliko watoto wa kipato cha kati katika nchi za magharibi"

Akielezea kumhusu mmoja wa waathiriwa wa unyanyasaji, alijisifu akisema "Nilimharibu msichana wa miaka 3 ambaye alikuwa amenipenda kama mbwa wangu na hakuna yeyote aliyejali ."

Mwaka jana BBC ilianda kipindi maalum kumuhusu Huckle, kilichofichua uhalifu wake miongoni mwa watoto nchini Cambodia, India na Uingereza.
Chanzo -BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527