BUNGE LAIAMURU IKULU YA MAREKANI KUTOA NYARAKA ZOTE ZA MAWASILIANO YA TRUMP

Kamati za Bunge la Marekani zinazoendesha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump zimeiamuru Ikulu ya Marekani (White House) kuwasilisha nyaraka zote za mawasiliano kati ya Rais Donald Trump na Ukraine.

Amri hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya Marekani kushindwa kuchapisha kwa hiari nyaraka hizo kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliokuwa umetolewa wa hadi Ijumaa.

Mmoja wa viongozi wa Kamati za Bunge amesema ni wazi Rais Trump amechagua njia ya kuficha ukweli baada ya kushindwa kwa mwezi mzima kuweka wazi nyaraka za mawasiliano yake na Ukraine.

Trump amesema huenda asitoe ushirikiano kwenye uchunguzi dhidi yake ambao unahusu madai kwamba alimshinikiza Rais wa Ukraine kumchunguza makamu wa Rais wa zamani, Joe Biden na mwanawe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527