MAZUNGUMZO YA MPANGO WA NYUKLIA KATI YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI YAVUNJIKA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 6, 2019

MAZUNGUMZO YA MPANGO WA NYUKLIA KATI YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI YAVUNJIKA

  Malunde       Sunday, October 6, 2019

Mwakilishi wa Korea Kaskazini katika mazungumzo ya mpango wa nyuklia yaliyofayika nchini Sweden, Kim Myong Gil amesema majadiliano kati ya nchi yake na Marekani yamevunjika. 

Mwakililishi huyo wa Korea Kaskazini amesema Marekani haijabadilika na wala haiko tayari kuacha tabia na mtazamo wake wa awali. 

Kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Morgan Ortagus amesema maoni ya Gil hayaakisi maudhui ya mazungumzo hayo. 

Majadiliano kati ya mataifa hayo mawili ni ya kwanza, tangu Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walipokutana mwezi Juni na kukubaliana kuanza tena mazungumzo baada ya majadiliano ya awali kukwama mwezi Februari mwaka huu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post