ATIWA MBARONI NA TAKUKURU KWA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA MILIONI 15


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mjini Dodoma imemkamata mratibu  wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) Wilaya ya Bahi, Emmanuel Mziwanda (62) kwa tuhuma za kuisababisha Serikali hasara ya Sh15 milioni.

Mkuu wa taasisi hiyo mjini humo, Sosthenes Kibwengo akizungumza leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa akiwa msibani alikuwa akitafutwa na taasisi hiyo tangu Julai,  2017 akikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka na kumdanganya mwajiri wake.

Amesema kitendo hicho kimeisababishia Serikali hasara ya Sh15 milioni na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika  na mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani, mtuhumiwa alitoweka kusikojulikana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527