ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), MICHAEL WAMBURA AOMBA MSAMAHA NA KUKIRI MAKOSA KWA DPP | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 2, 2019

ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), MICHAEL WAMBURA AOMBA MSAMAHA NA KUKIRI MAKOSA KWA DPP

  Malunde       Wednesday, October 2, 2019

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yake.

Wambura alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11 mwaka huu akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Tsh.Mil 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.

Hayo yamebainika mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya Wambura kueleza kuwa ameandika barua kwa DPP ili kuomba msamaha na kukiri makosa yake hivyo anauomba upande wa mashtaka kufuatilia ili aweze kupata haki yake.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post