WAZIRI LUGOLA AMTAKA RPC MOROGORO ARUDI KILIMANJARO HARAKA


WAZIRI  wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Hamis Issa kurudi Mkoani Kilimanjaro na kuhakikisha Mwananchi Hemed Mbaga anatolewa mahabusu kutokana na kubambikiziwa kesi.

Pia amemwagiza OCD wa Dodoma Mjini, Joas Steven kumpa orodha ya askari ambao wamekuwa wakiwabambikizia kesi madereva  bodaboda na bajaji wa Dodoma ili aanze kushughulika nao.

Lugola ametoa agizo hilo jana Septemba 22,2019 katika bonanza lililofanyika uwanja wa shule ya msingi Chang'ombe jijini Dodoma baada ya  kukutana na waendesha bodaboda na bajaji ili kusikiliza kero zao.

Waziri Lugola amesema Julai  18,2019 Polisi mkoani Kilimanjaro walimkamata Mbaga wakati alipokwenda kuangalia mkusanyiko wa watu kufuatia bodaboda wawili kutelekeza furushi la bangi.

"Maofisa wa halmashauri walikuwa wanapita hapo kuelekea kwenye makusanyo lakini walikuwa wa kwanza kufika na ndipo Mbaga akaja akitokea nyumbani lakini cha ajabu wakambambikiza kesi na kumuweka mahabusu hadi leo," amesema Lugola.

Kwa mujibu wa Waziri, taarifa zilimfikia na akaagiza mtuhumiwa atolewe haraka mahabusu lakini cha ajabu hadi jana alikuwa hajatolewa huku RPC akihamishiwa Morogoro.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527