TGNP: VYOMBO VYA HABARI VIELIMISHE WANANCHI KUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU NA SERIKALI ZA MITAA


Vyombo vya habari nchini Tanzania vimetakiwa kuwaelimisha wananchi kuuelewa mchakato wa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa kwaka huu ili watambue wajibu wao katika masuala ya uchaguzi.


Rai hiyo imetolewa leo Jumanne Septemba 17,2019 na  Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius  Temba wakati wa warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii kuhusu wanawake na uongozi inayolenga kuwajengea na kuwaongezea uelewa na uwezo waandishi wa habari namna ya kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye nafasi za uongozi.

"Vyombo vya habari vina wajibu wa kuhabarisha wananchi kuhusu mchakato wa uchaguzi,ushiriki wa wananchi kwenye mchakato wa uchaguzi ili washiriki kikamilifu na wawe na maamuzi sahihi",amesema Temba.

Temba ametumia fursa hiyo kuwahamasisha waandishi wa habari kuandika habari kwa kuzingatia mrengo wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kuzielewa kanuni za uchaguzi sambamba na majukumu yao ili wasiachwe nyuma.

"Misingi mikuu ya uandishi wa habari inatufundisha kuwa ili tuweze kufanya kazi kiuweledi ni lazima tuzingatie usahihi wa habari tunazoandika,uhuru,uwajibikaji,ubinadamu na kutopendelea upande wowote. Wakati wa kuandika habari za uchaguzi,vyombo vya habari vitumike kujenga uelewa,ujasiri na uthubutu wa wanawake katika uchaguzi",ameongeza Temba.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na UN Women imekutanisha  waandishi wa habari 43 kutoka mikoa mitano ambayo ni Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara.
Lengo kuu ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa zenye mrengo wa kijinsia hasa zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo kubadili mitazamo na mila hasi zinazozuia ushiriki wa wanawake katika uongozi.
 Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius  Temba akitoa mada kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki kwenye uongozi na ngazi za maamuzi na wajibu wa vyombo vya habari.  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius  Temba  akitoa mada kuhusu umuhimu wa wanawake kushiriki kwenye uongozi na ngazi za maamuzi na wajibu wa vyombo vya habari.
 Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akielezea misingi ya uandishi wa habari.
 Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao Deogratius Temba akielezea changamoto zinazowafanya wanawake wasishiriki kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ambazo ni Fikra mgando,kutojiamini,ukosefu wa rasilimali na ubaguzi wa kijinsia.

Mwenyekiti wa TAMWA,Joyce Shebe ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari,Clouds Media akitoa mada kuhusu uandishi wa habari kwa mrengo wa kijinsia.

Mwenyekiti wa TAMWA,Joyce Shebe ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari,Clouds Media akitoa mada kuhusu uandishi wa habari kwa mrengo wa kijinsia.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia : WAANDISHI WATAKIWA KUWA MABALOZI KUBADILI MIFUMO HASI INAYOKANDAMIZA WANAWAKE KWENYE UONGOZI

Soma pia : Picha : TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WANAWAKE NA UONGOZI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527