WAKAZI 60 MSALALA WAPATIWA KADI ZA CHF | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 13, 2019

WAKAZI 60 MSALALA WAPATIWA KADI ZA CHF

  Malunde       Friday, September 13, 2019
NA SALVATORY NTANDU

Kaya 12 zenye watu wenye ulemavu wa viungo mbalimbali katika kata za bugarama na Kakola katika Halamshauri ya Msalala zimepatiwa msaada wa kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) na kampuni ya Azan Logistic inayotekeleza zabuni zabuni ya kutoa taka ngumu katika mgodi wa Acacia Bulyankhulu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hizo Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu kata ya kakola, Emmanue Matiku ameshuishukuru kampuni hiyo kwa kuwapa msaada huo na kusema kuwa zitawasaidia kupata huduma za matibabu bure kwa mwaka mzima.

Amesema kadi hizo zitawawezesha walemavu zaidi 60 kupata matibabu bure kwa mwaka mzima hali ambayo itasaidia kupunguza adha katika kupata huduma za afya kutokana na wengi wao kukabiliwa na magonjwa mbalimbali katika maeneo yao wanayoishi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Said Azan Said amesema ameamua kutoa msaada huo ili kurudisha fadhila kwa jamii ambayo kamapuni yake inafanya kazi na kutoa rai kwa wawekezaji wengine kuiga mfano wake katika kuchangia shughuli za maendeleo.

Amesema Azan Logistic imetoa misaada mbalimbali ikwemo saruji mifuko 30 na tofali 2000 katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha kakola,hundi ya shilingi milioni 3 katika ujenzi wa jengo la kituo cha polisi Bugarama,ajira vijana 28 na walimu wawili wa masomo ya sayansi pamoja na kadi hizo za CHF.

Azan amefafanua kuwa msaada huo unathamini ya shilingi milioni 56 na ni sehemu ya ahadi yake alioitoa kwa wakazi wa vijiji vya kakola na bugarama baada ya kupata zabuni ya kutoa taka ngumu katika mgodi wa Acacia Bulyankhulu ya miaka miwili.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Anamringi Macha ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo na kutoa rai kwa wawekezaji wengine katika wilaya hiyo kushiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kutimiza ahadi mbalimbali wanazo ziahidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama  Anamringi Macha amewataka wawekezaji wilayani humu kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutatua kero zilizopo katika maeneo yao ya uwekezaji sambamba na kutoa  ajira kwa vijana.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post