Juliana Shonza : Serikali inaendelea kusajili vyama na vilabu vya michezo kwa wanawake.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM  
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea kusajili Vyama na Vilabu vya michezo ikiwemo vya soka la wanawake ili kuimarisha maendeleo ya mchezo huo chini. 

Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe.Devotha Minja (Viti Maalum) aliyeuliza Je ni upi mkakati wa Serikali wa kuhamasisha soka kwa wanawake katika ngazi za Mikoa na Wilaya kuwa na timu za soka kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume ? 


“Serikali imekuwa ikiandaa program mbalimbali za kukuza na kuendeleza soka la wanawake ikiwemo michezo ya UMITASHUNTA na UMISETA na  kuanzishwa kwa shule za michezo ambazo zinadahili wanamichezo wa kike ambao moja kati ya michezo inayofundishwa ni mpira wa miguu”amesema Mhe.Shonza. 


Akijibu maswali ya nyongeza ya Wabunge Mhe.Shonza ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wafadhili na wadhamini mbalimbali kufadhili na kudhamini soka la wanawake nchini. 


Aidha Mhe.Shonza amesema kuwa mafunzo mbalimbali ya ukocha na uamuzi wa mpira wa miguu kwa wanawake yameendelea kutolewa,sasa tunawaamuzi wanaotambulika na Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) 


Halikadhalika Mhe.Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea kuwahamasisha wanawake kujihusisha katika kucheza mpira wa miguu kwa kuwa ni mchezo maarufu na kwamba unatoa fursa ya ajira kwa mtoto wa kike. 


…MWISHO..


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post