UFUKWE WA COCO BEACH WATEKETEA KWA MOTO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 22, 2019

UFUKWE WA COCO BEACH WATEKETEA KWA MOTO

  Malunde       Sunday, September 22, 2019
Eneo la starehe (Pub) lililoko kwenye ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam, limetekea kwa moto huku chanzo cha moto, kikiwa bado hakijajulikana.
Eneo hilo ambalo lipo Msasani jijini Dar es salaam linatajwa kuanza kuungua kwa moto, majira ya saa 7 mchana, ambapo kwa mujibu wa Meneja Pub hiyo, Davis Urasa mpaka sasa bado hawajatambua hasara kiasi gani iliyotokea.

"Kama mnavyoona kuna moto umetokea hapa na ulianza majira ya saa 7 mchana, na tulianza kuona moshi ukitokea juu baada ya hapo muhusika wa umeme alijaribu kwenda kuzima, japo hatukufanikiwa" amesema Meneja Davis Urasa

"Mpaka sasa kiundani bado hatujajua chanzo ni nini, tunasubiri taarifa kutoka kwa Polisi wajaribu kutueleza" amesema Meneja wa Pub hiyo Samia Rajab

Kamanda wa Polisi Mussa Taibu, amesema na wao wamepokea taarifa hizo na wamefanya juhudi za awali za kuhakikisha moto huo unazimwa, na sasa wanafuatilia chanzo ni nini.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post