TRUMP ATHIBITISHA KIFO CHA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN


Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliuawa katika operesheni ya Marekani.

Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.

Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita. Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.

Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.

''Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan / Pakistan''.Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu ya Whitehouse.

Taarifa hiyo haikutoa mda wa operesheni hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527