SAUDI ARABIA YASITISHA SHUGHULI KATIKA VITUO VYA MAFUTA VILIVYOSHAMBULIWA NA WAASI WA YEMAN | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 15, 2019

SAUDI ARABIA YASITISHA SHUGHULI KATIKA VITUO VYA MAFUTA VILIVYOSHAMBULIWA NA WAASI WA YEMAN

  Malunde       Sunday, September 15, 2019
Saudi Arabia imesitisha kwa muda uchimbaji mafuta katika vituo viwili ambavyo vimeshambuliwa na ambavyo vinamilikiwa na kampuni ya mafuta ya nchi hiyo Saudi Aramco.


 Waziri wa nishati ambaye pia ni mwanamfalme Abdulaziz bin Salman amesema hayo jana kupitia taarifa, na kuongeza kuwa kufuatia mashambulizi hayo, uchimbaji mafuta katika vituo hivyo umepungua kwa asilimia 50. 

Waasi wa Houthi wenye mafungamano na Iran wamethibitisha juu ya kurusha ndege 10 zisizokuwa na rubani zilizoshambulia vituo hivyo vya mafuta. 

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani  ya Saudi Arabia, hujuma hizo zimesababisha moto katika vituo hivyo. 

Msemaji wa wanamgambo wa Yemen amesema shambulio hilo "ni jibu" kwa operesheni za kijeshi zinazoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Wahouthi nchini Yemen. 

Marekani imeituhumu Iran kwa kuhusika na mashambulizi hayo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post