NYOKA ANAYEDAIWA KUGAWA BARAKA GEITA AHAMISHIWA KAHAMA


Wananchi wakiwa wamembeba nyoka aina ya Chatu anaedaiwa kuwa wa bahati kutokana na upole wake aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato 

Anaandika Rehema Matowo wa Mwananchi 

 Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa) imemchukua nyoka mkubwa aina ya chatu aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi wilayani Kahama kuhifadhiwa.

Nyoka huyo anayeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 11, 2019 amesema Tawa iliwatafuta wataalam wa nyoka kutoka makumbusho ya Bujora waliofanikisha kumchukua noka huyo aliyekuwa katika kichuguu akiwa amelalia mayai 20.

Mmoja wa Wananchi wa kijiji hicho, Philipo Maduhu amesema nyoka huyo ni baraka kwao na halmashauri haikupaswa kumuondoa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527