IGP SIMON SIRRO ALIVYOKABIDHIWA BENDERA NA KUWA MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI MASHARIKI MWA AFRIKA EAPCCO

IGP Simon Sirro amekabidhiwa bendera na kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika EAPCCO. 

Umoja huo unaundwa na nchi za Burundi, Comoros, Djibouti, DRC, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, South Sudan, Sudan, Tanzania na Uganda.
IGP wa Sudan Adil Mohamed Ahmed, akikabidhiwa bendera ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika ili aweze kumkabidhi IGP Sirro, ishara ya kumwachia kijiti cha uenyekiti wa Shirikisho kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ni miongoni mwa wanaoshuhudia IGP Sirro akikabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika kutoka kwa IGP wa Sudan (PICHA- Jeshi la Polisi)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527