HARMONIZE AFUNGA NDOA KISIRI BILA WASAFI



Nchini Tanzania, msanii Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake ambaye ni raia wa Italia, Sarah Michelotti siku chache baada ya mwanamuziki huyo kujiondoa rasmi katika kundi la Wasafi Classic Baby WCB ambalo linaongozwa na msanii kinara nchini Tanzania, Diamond Platnums.

Mwanamuziki huyo anayependa kujiita konde boy akimaanisha kuwakilisha wamakonde kutoka kusini mwa Tanzania alimchumbia Sarah miezi michache iliyopita na hakuwahi kutangaza siku rasmi ya harusi yake.

Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri ilifanyika jumamosi ya tarehe 7, Septemba 2019 jijini Dar es salaam na kuhudhuria na wageni 100 tu.

Si jambo la kawaida kwa harusi nchini Tanzania kuhudhuriwa na watu wachache kiasi hicho hata kwa watu ambao si maarufu.

Gazeti la The Citizen nchini Tanzania limeandika kuwa hakuna msanii hata mmoja kutoka kundi lake la zamani la Wasafi aliyeudhuria tafrija hiyo ya mwana muziki huyo.

Pongezi nyingi kwake zimetoka kwa mashabiki na wadau wa tasnia kwa hatua ambayo amepiga na kutajwa kuwa mfano wa kuigwa

Wakati harusi hiyo ikiwashangaza wengi katika mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuwa labda ndoa ndio ilikuwa sababu kuu ya mwanamuziki huyo kuacha kuimba na Diamond.
Harmonize kwa sasa anasifika kwa wimbo unaompongeza rais Magufuli katika utendaji wake wa kulijenga taifa unaoitwa 'magufuli'.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527