KUTANA NA MZEE AMBAYE HAJAWAHI KULA WALA KUNYWA MWAKA WA 70 SASA


Prahlad Jani
Kuna mambo ukiambiwa unaweza usiamini sababu ni tofauti kabisa na namna unavyofahamu wewe au ilivyokawaida.

Nchini India kuna mzee ambaye unaambiwa hajawahi kula wala kunywa maji kwa zaidi ya miaka 70.

Pengine ni jambo kubwa sana la kushangaza, inakuaje mtu hajala wala kunywa kwa miaka yote hiyo, wakati inafahamika kuwa kwa binadamu wa kawaida kama atakosa chakula na maji ndani ya siku tatu anaweza kufa.

Mzee Prahlad Jani amezaliwa mwaka 1929 na anasema hajawahi kugusa kitu chochote tangu mwaka 1940 mpaka sasa.

INAKUAJE MPAKA SASA YUPO HAI?

Kwa maelezo yake mwenyewe Prahlad anasema anapata nguvu kutoka kwa Mungu wake anayefahamika kwa jina la Amba' ambaye ndiye aliyempa muujiza huo na pale anapokuwa anasikia njaa kuna tundu dogo katika mdomo wake juu karibu na matundu ya pua, tundu hilo humpatia kitu kama mate mate yanayomfanya asisikie kutumia kitu chochote kile pale anaposikia njaa.

Mwaka 2003 alifanyiwa vipimo na madaktari ili kugundua ukweli wa jambo hilo kwa siku 10, madaktari wanasema kuwa katika siku hizo hawakuwahi kumuona akipata chakula au kunywa maji na uchunguzi wa mwili wake ulionesha uko vizuri kama mtu wa kawaida.

Haja ndogo yake ilionesha kutengenezwa katika kibofu lakini ilikuwa ikifyonzwa na mwili wake, jambo ambalo sio kawaida na kingine walichoona zaidi ni tundu dogo ndani ya mdomo juu kidogo karibu na matundu ya pua.

Mwaka 2010 utafiti mwingine tena ulifanyika na majibu waliyopata yalikua ni hayo hayo, mzee Prahlad hawakuwahi kumuona kwenda chooni au kula chochote.

Vyanzo: Lightdocumentary.com, Wikiversity.org

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post