MWANAMKE AFUNGA NDOA NA MTI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 14, 2019

MWANAMKE AFUNGA NDOA NA MTI

  Malunde       Saturday, September 14, 2019
Mwanamke mwenye umri wa miaka 34 na ambaye pia ni mama wa watoto wawili 'amefunga' ndoa na mti katika eneo la Rimrose Valley Park, Merseyside, Uingereza.

 Harusi hiyo ya kushangaza imefanyika mnamo Septemba 7, 2019 huku ndugu, jamaa na marafiki wakijitokeza kushereherekea hafla hiyo. 

Bi harusi Cate Cannigham alivalia rinda la kijani kibichi wakati wa harusi hiyo.  

Ripoti zilisema kuwa Cunnigham ambaye ni mtaalamu wa mazingira aliamua kufunga ndoa na mti ili kupinga ujenzi wa barabara katika bustani hiyo.

Picha ambazo zimekuwa zikisambazawa mitandaoni zimefichua umbali ambao mwanadamu anaweza kufika kulinda uhai wa miti. 

Baada ya kupata 'mume' mwanamke huyo alibadilisha jina lake na kujiita Cate Rose Elder,jina ambalo alilihusisha na mume wake mpya. 

 Mama huyo wa watoto wawili alisaidiwa na mchumba wake katika mipango ya kuandaa harusi hiyo kando na kuihudhuria pia.

Inasemekana kuwa wakazi wa eneo hilo walikuwa wakilalamikia mipango ya ujenzi wa barabara inayopaswa kupitia katikati mwa bustani hiyo wakisema kuwa itaharibu mazingira hayo.

 Wakazi wanaamini hatua ya Cunningham itasitisha shughuli hiyo. 

'Harusi' hiyo ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa Canningham. 

Kisa sawia na hicho kilishuhudiwa huko Florida baada ya mwanamke aliyetambulika kama Karen Cooper kufunga ndoa na mti mkubwa ulioishi kwa takriban karne moja. 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post