MARAIS 10 WASHIRIKI MAZISHI YA ROBERT MUGABE | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 14, 2019

MARAIS 10 WASHIRIKI MAZISHI YA ROBERT MUGABE

  Malunde       Saturday, September 14, 2019

 Marais wa nchi 10 barani Afrika, pamoja na waliostaafu leo Jumamosi Septemba 14, 2019 wameshiriki mazishi ya Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

Mwili wa mwanamapinduzi huyo aliyefariki Septemba 6, 2019 nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu unaagwa leo katika uwanja wa Harare.

Marais hao ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta; Rais wa Zambia, Edgar Lungu; Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi; Rais wa Namibia, Hage Geingob; Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Mbasogo; Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa; Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina; Rais wa Malawi, Peter Mutharika, Rais wa Angola, João Lourenço na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.

Rais wa Singapore, Halimah Jacob naye ameshiriki mazishi hayo.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post