MZOZO WAIBUKA MAZISHI YA ROBERT MUGABE...FAMILIA YAGOMA KUZIKWA MAKABURI YA MASHUJAAFamilia ya kiongozi wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe imekataa shujaa huyo wa vita vya ukombozi kuzikwa katika makaburi ya kitaifa ya mashujaa na badala yake wanataka azikwe katika makaburi ya familia kama alivyousia wakati wa uhai wake.

Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe unatarajiwa kuwasili Jumatano nchini Zimbabwe na serikali imethibitishwa kuwa mazishi yake yatafanyika katika siku mbili za wikendi ijayo.

Mugabe alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, akiwa hospitalini Singapore wiki iliyopita

Lakini sasa inaonekana kuna mzozo wa kutoelewana baina ya familia ya marehemu Mugabe na serikali ya Zimbabwe kuhusu ni wapi kiongozi huyo aliyeitawala Zimbabwe kwa miaka 37 kuanzia 1980 hadi 2017, anapaswa kuzikwa.

Baadhi ya ndugu zake wanataka azikwe katika kijijini alikozaliwa cha Kutama kilichopo katika jimbo la magharibi la Mashonaland yapata kilomita 80 au maili 50 magharibi mwa mji mkuu Harare.

Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.

Mpwa wa Mugabe anasema alikuwa akiwa mtu mwenye machungu kutokana na usaliti aliofanyiwa na watu wake wa karibu

Ndani ya lango la nyumba ya Mugabe ya kijijini kwao , ambayo kwa sasa inalindwa na mlinzi mmoja, makumi kadhaa ya waombolezaji walikusanyika Jumapili kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Mugabe.

Waliketi kwenye makundi madogo madogo, huku wakiongea kwa sauti ya chini. Kulikuwa na hali ya wasi wasi - kuashiria kuwa mambo yalikuwa sio mazuri.

Katika mojawapo ya vyumba vya nyumba hiyo, wazee wa kijiji, na machifu walikuwa wakiamua ni wapi Mugabe angezikwa.

Mpwa wake , Leo Mugabe, amekanusha kuwa kuwa kulikuwa na suala la kutoelewana na serikali, lakini akakiri kuwa mjomba wake alikufa akiwa mtu mwenye hasira sana baada ya kung'olewa madarakani mwaka 2017 na jeshi pamoja na makamu wake wa zamani.

"Alikuwa mwenye machungu ...Unaweza kufikiria watu ambao uliwaamini- watu ambao walikuwa wakikulinda,wakikushughulikia, usalama wako unakugeuka. Alikuwa mwenye masikitiko makubwa na iliweka doa kwenye utawala wake ," alisema.
Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa

Father Fidelis Mukonori, ambaye alikuwa na jukumu muhimu katika mazungukati ya waliopanga mapinduzi ya mwaka 2017 na Bwana Mugabe ,anasema kuwa anatamani angekuwa memuomba rafiki yake angekuwa amemuombea rafiki yake miaka 40 kama kweli alihisi kuwa maesalitiwa.

"Ninajihisi mzito sana ndani yangu kwasababu unaweza kumpata baba mmoja tu wa taifa - kama mtoto unaweza kuwa na wazazi tu. Ameondoka."

Kasisi wa Kikatoliki anasema kuwa Bwana Mugabe ni roho ya watu 70 000 waliokufa wakati wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe.

Lakini kasisi huyo anamatumaini juu ya namna kiongozi huyo aliyewaongoza Wazimbabwe kupata uhuru alivyohisi kabla ya kifo chake : "Alikuwa tayari kuondoka , alikuwa na utashi wa kuondoka, alikuwa ana matumaini ya kuondoka."

Wakuu wa mataifa wanaalikwa katika sherehe za umma za kutoa heshima kwa Bwana Mugabe, lakini si kwa ajili ya mazishi halisi.
CHANZO -BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post