WAZAZI WANAORUBUNI WATOTO WAFANYE VIBAYA KWENYE MITIHANI WAONYWA KAGERA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Murshid Hashimu Ngeze 

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog  Kagera
Wazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuwavunja moyo watoto wao hasa wanafunzi wanapokaribia kufanya mitihani yao ya taifa kwa kuwatka wafanye vibaya kwenye mitihani.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 3, 2019 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Murshid Hashimu Ngeze katika kuelekea kufanya mitihani ya Taifa kwa wanafunzi wa shule ya msingi kote nchini wiki ijayo.

Ngeze amesema kuwa kitendo hicho cha mzazi au mlezi kumtamkia mwanaye kuwa afanye vibaya kwenye mtihani ili ashindwe ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha juhudi na ndoto za mtoto katika kufikia malengo yake katika maisha.

Mwenyekiti huyo amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kutoongea na watoto wao hasa mabinti katika misingi iliyo bora, hivyo amewahimza wazazi na walezi kununua vifaa muhimu vya watoto ili kunufaika na elimu bure inayotolewa nchini.

Aidha Ngeze amekemea tabia za baadhi ya waendesha bodaboda wanaowadanyanya wanafunzi kwa kuwarubuni kwa zawadi na lifti, kuwa tabia hiyo sio nzuri ambapo tayari mikakati mbalimbali inafanyika ili kupambana na vitendo hivyo ambavyo huwafanya wanafunzi kukatisha masomo kwa kupata ujauzito na kushinddwa kufikia malengo yao.

Aidha amemshukuru  Rais John Magufuli kwa kitendo cha kuwaita Ikulu maafisa watendaji wa kata kote nchini kwa lengo la kuzungumza nao kwa kuwapa maelekezo ya kuijenga nchi.

Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kushiriki katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ukamlifu na kuguswa na miradi hiyo ambapo hadi sasa ameitaja Halmashauri hiyo kuwa katika hatua nzuri kwani miradi mingi inaendelea kutekelezwa ambapo usimamizi wa fedha ni mzuri.

Amesema serikali hutumia fedha nyingi katika miradi ya maendeleo kwa wananchi hivyo ni vema miradi hiyo itunzwe na kulindwa huku akiwataka wananchi kutoa taarifa mara moja pale wanapogundua au kubaini baadhi ya watu wanaohujumu miradi hiyo ili hatua kali ichukuliwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post