MSHTAKIWA ADAI SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZIMETOWEKA KIMAAJABU BAADA YA KUTEMBEA NA MTOTO WA SHEIKH

Mshtakiwa Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba Mahakama imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo kupata maumivu makali anapokuwa Mahabusu.


"Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mtoto wa Shekhe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na Binti yake lakini sikusikia ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamha kutuliza maumivu"-Alisema

Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.

Hata hivyo Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi, Kesi imeahirishwa hadi September 27 mwaka huu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527