MTOTO WA MKUU WA MAJESHI TANZANIA AFARIKI KWA AJALI YA NDEGE


Nelson Mabeyo, mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ni miongoni mwa watu wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Auric iliyotokea leo asubuhi Jumatatu Septemba 23,  2019.

Nelson ndio  alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ndege hiyo ilianguka  asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527