ALIYELALA AKIOTA ANAMEZA PETE YA UCHUMBA AAMKA NA KUKUTA KWELI KAIMEZA

Jenna Evans aliyemeza pete ndotoni


Mwanamke mmoja nchini Marekani amewashangaza wengi baada ya kumeza pete ya uchumba iliyokuwa kidoleni akiwa amelala fofofo na alipoamka katika nyumba yake California aligundua kuwa alichofikiria kilikuwa ni ndoto tu, lakini baadaye akagundua kuwa pete yake haipo kidoleni.

 Jenna Evans, mwenye umri wa miaka 29, sasa amelazimika kufanyiwa upasuaji kuondoa pete hiyo tumbani. 

 Kulingana na ripoti ya ABC news, aliota kuwa, mchumba wake Bobby Howell alikuwa katika treni ya mwendo kasi na akalazimika kumeza pete ili kuilinda dhidi ya “watu wabaya”. 

Alipoamka katika nyumba yake California aligundua kuwa alichofikiria kilikuwa ni ndoto tu, lakini baadaye akagundua kuwa pete yake haipo kidoleni.

Upasuaji ulikuwa wa mafanikio, na Evans alilia sana baada ya kugutuka kutoka usingizini mara baada ya pete kuondolewa tumboni.

Evans ambaye ni mkazi wa San Diego alisema kuwa, alipogundua hana pete hiyo alimwamsha Bobby kumweleza, na ndipo wakashauriana na hatimaye wakaenda hospitalini.

 Hospitalini, picha za skani ya X-ray zilibaini kuwa ni kweli pete hiyo ilikuwa tumboni, na madaktari wakakubaliana kuwa lingekuwa si jambo la busara ”kuiacha itoke yenyewe kwa njia ya choo” 

Baadaye, Evans alifanyiwa upasuaji na pete hiyo kuondolewa. 

“Halafu nikalia sana kwa sababu ningekuwa mjinga sana kama ningekufa. Niliisubiri sana pete hii ya uchumba na nitaolewa na Bobby Howell.” alisema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, upasuaji ulikuwa wa mafanikio, na Evans alilia sana baada ya kugutuka kutoka usingizini mara baada ya pete kuondolewa tumboni. “Nilifurahi sana kwa sababu nisingewezatena kuiangalia na kuithamini kama ilivyokuwa awali, iliwa ningeiacha itokee kwa njia ya choo” aliongeza kusema. 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527