WACHIMBAJI 10 WA MADINI WAFUKIWA NA KIFUSI MISUNGWI


Picha haihusiani na tukio halisi lililotokea

Takribani watu wanane kati ya 10 ambao ni wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Shilalo ulioko katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wameokolewa wakiwa hai, baada ya kufukiwa na kifusi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro, amesema kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa 7:00 leo usiku mara baada ya shimo namba 47 waliloingia kuelemewa na udongo na kisha kuporomoka.

''Baada ya tukio hilo kutokea, jitihada mbalimbali zilifanyika na kufanikiwa kuwaokoa watu wanane wakiwa hai, wawili wakawa bado ila baadaye mmoja aliokolewa akiwa amefariki tayari na juhudi hadi sasa zinaendelea ili kumuokoa huyo mmoja aliyebakia''. amesema Kamanda Muliro.

Kamanda Muliro ameongeza kuwa manusra wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kutoa wito kwa wachimbaji wadogo wadogo kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uangalifu zaidi.
Via>>EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527