FACEBOOK KUKABILIANA NA AKAUNTI FEKI ZA WATUMIAJI

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amekuwa akipambana kudhibiti habari za uongo kwa miezi ya hivi karibuni

Mtandao wa Facebook umesema umeanzisha upelelezi kukabiliana na akaunti feki za watumiaji.

Tiyari umeshaanza kutumia wafanyakazi kutoka nje ya kampuni hiyo watakaoweza kugundua kompyuta zinazotumika mara kwa mara ambazo zinahusiana na akaunti hizo.

Facebook wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya wale wanaoghushi habari kwa kutumia akaunti hizo ikiwemo mtu mmoja aliyewahi kudanganya kuwepo kwa mwizi aliyekuwa na silaha ya moto katika mgahawa mmoja mjini Washington taarifa ambazo hazikuwa na ukweli wowote.

Inasemekana kuwa baadhi ya watu hutumia pia akaunti feki kuweka habari kwenye facebook ili wapate watizamaji wengi na hivyo kuongeza fedha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527