MWANAJESHI AKAMATWA KWA KUFUNDISHA WATU KUTENGENEZA MABOMU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 25, 2019

MWANAJESHI AKAMATWA KWA KUFUNDISHA WATU KUTENGENEZA MABOMU

  Malunde       Wednesday, September 25, 2019
Shirika la FBI limemkamata mwanajeshi wa Marekani kwa kutuhumiwa kusambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii ya namna ya kutengeneza mabomu.

Jarrett William Smith anatuhumiwakupendekeza kutumia bomu la kwenye gari kushambulia kituo kikubwa cha habari Marekani.

Mwanajeshi huyo mwenye miaka 24 aliandika katika mtandao wa kijamii kwamba angetaka kulipigania kundi la wafuasi wa mrengo wa kulia nchini Ukraine wanedehsa mashtaka wamesema.

Alipendekeza kuwa angewaua wafuasi wa kundi la mrengo wa kushoto Antifa, linasema FBI.

Alikamatwa mwishoni mwa juma na kushtakiwa kwa kusambaza taarifa zinaozhusiana na silaha za kuangamiza umma.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani, Smith aliwasiliana tangu 2016 na raia mwingine wa Marekani aliyesafiri kwenda Ukraine kupigana na kundi la utaifa, the Right Sector.

Inaarifiwa kuwa Smith alijadiliana na Lang kwenye Facebook kuhusu namna ya kuunda mabomu.

"Ni kweli nilipata elimu kuhusu mabomu ya IED kwa siku kadhaa," amesema Smith katika mawasiliana hayo mnamo Desemba 8 2018, kwa mujibu wa nyaraka hizo.

"Tunaweza kutengeneza mabomu ya simu kama yanayotumika Afghanistan. Ninaweza kukufunza hilo."

Mshukiwa alikuwa anatafuta wengine 'wenye itikadi kali'

Katika mawasiliano yaliofuata katika mtandao wa kijamii na duru kutoka FBI mwezi Agosit na Septemba kupitia mtandao wa Telegram, Smith alizunguma kuhusu kutengeneza bomu kubwa la kwenye gari kushambulia makao makuu ya vituo vya habari Marekani.

Mnamo Agosti 19 August, inadaiwa Smith alimuambia afisa huyo wa FBI kuwa anatafuta watu wengine 'wenye itikadi kali' kama yeye.

Siku mbili baadaya alijadili namna ya kuunda mabomu kutokana na vifaa vilivyopo ndani ya nyumba.

Alitoa vidokezo vya nmna ya kuunda vilipuzi vinavyoweza kulipuliwa kwa simu ya mkononi.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, mshukiwa amekiri kutoa taarifa kwa watu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu namna ya kuunda mabomu.

Alisema kuwa alitoa mafunzo hayo ili 'azushe ghasia', wachunguzi wanasema.

Smith anakabiliwa na hadi miaka 20 gerezani iwapo atapatikana na hatia.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post