ASKOFU MKUU YUDA THADEUS RUWA'ICHI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI MOI LEO.....AMSHUKURU RAIS MAGUFULI NA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. 


Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). 

Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu 

Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019.


Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu.


Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.

PICHA NA ISSA MICHUZI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527