BASHE ASEMA KUNA UPOTEVU WA ZAIDI YA BILIONI 120 KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA


Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.

“Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote,” amesema.

“Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua,” amesema Bashe.

Aidha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi  kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527