KIJANA ALIYEJIFANYA BABU WA MIAKA 81 AKAMATWAJayesh Patel akiwa amevalia kilemba na ndevu nyeupe
Patel alipokuwa kwenye kiti chake cha magurudumu akifanyiwa uchunguzi.
Patel alipatikana kuwa na pasipoti feki na kuzuiliwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa ndege
Jayesh Patel

Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi jijini New Delhi, wamemkamata mwanamume mmoja katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi nchini India, kwa kujifanya kuwa mzee wa miaka 81 ili kusafiri kwenda nchini Marekani.

 Jayesh Patel aliwasili katika uwanja huo mnamo Jumapili, Septemba 8,2019 huku akijiendesha kwenye kiti cha magurudumu na kupaka rangi ndevu zake kuwa nyeupe na kuvalia macho nne na kilemba kichwani tayari kuabiri ndege ya kuelekea New York. 

Patel aliwasili kwenye uwanja huo wa ndege akiwa amevalia kilemba, macho nne na ndevu nyeupe. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Times if India, mambo yote yalikuwa yakionekana kuwa shwari kwa Patel hadi pale aliagizwa kusimama ili kuchunguzwa. 

"Afisa wetu alimuagiza mtu huyo aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu kusimama. Alisema hawezi kusimama. Kisha afisa wetu akamuagiza endapo anaweza kusimama kwa kusaidiwa. Lakini alisitasita akisimama," alisema Shrikant Kishore, ambaye ni afisa mkuu wa Central Industrial Security Force.

 Ni katika harakati hiyo ndipo maafisa wa uwanja huo wa ndege kutambua kuwa nywele na ndevu za msafiri huyo zilikuwa nyeupe na mizizi yake zikiwa nyeusi.

 Jamaa huyo pia alikuwa akizikwepa macho za maafisa hao. 


Wakati alipoulizwa pasipoti yake, Patel aliwasilisha stakabathi zilizokuwa zikimtambua kama Amrick Singh, aliyezaliwa jijini Delhi mwezi Februari mwaka 1938, na kumfanya kuwa babu wa miaka 81.

 "Kwa kweli hakuwa mzee wa miaka 80. Ngozi yake ilikuwa ya kijana," alisema Kishore. 

Baada ya kuhojiwa zaidi, aliwaambia maafisa hao wa usalama kuwa jina lake ni Jayesh Patel, na ana umri wa miaka 32, mkazi wa Gujarat.

 Patel alipatikana kuwa na pasipoti feki na kuzuiliwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa ndege kisha kuwasilishwa kwa maafisa wa idara ya uhamiaji kwa udanganyifu.

 Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Indira Gandhi, ambayo inatambulika sana kama uwanja wa Delhi, ni ya 12 ulimwenguni kwa kuwa na wasafiri zaidi ya 70 milioni waliosafiri mwaka 2018. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post