FILAMU YA MIMI SIYO MWEHU KUZINDULIWA RASMI JUMATANO SEPTEMBA 18,2019

Unaikumbuka ile Filamu ya Laana ya Mke iliyoigizwa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga ambayo hivi karibuni ilifanikiwa kushinda Tuzo ya Heshima Filamu Bora yenye maudhui ya kitaifa Kanda ya Ziwa???.



Sasa ni hivi?!! Baada ya Filamu ya Laana ya Mke kutikisa....Wasanii wa Filamu mkoa wa Shinyanga wanakuletea filamu nyingine kali itazinduliwa Siku ya Jumatano Septemba 18,2019  imepewa jina la " MIMI SIYO MWEHU".... Ndiyo!! Mimi siyo Mwehu ni bonge la filamu yenye tungo zenye manufaa katika jamii zenye kuelimisha, kuonya,kuburudisha zilizojaa mafunzo ya uhalisia wa maisha halisi katika jamii za Kiafrika.

Mwandaaji wa Filamu hiyo, Ibrahim Juma Songoro maarufu 'Songoro Gadafi' ambaye ni Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga ameiambia Malunde1 blog kuwa filamu ya 'Mimi Siyo Mwehu' inalenga kuelimisha jamii inayowachukulia watu wasio na kipato,waliochoka kimaisha, kiuchumi na kiafya mawazo yao au ushauri wao haustahili bali ni wendawazimu.

"Tunapenda kuwataarifu wadau wa Filamu kuwa Bongo Movies shinyanga itazindua Filamu ya Mimi Sio Mwehu Septemba 18,2019 katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga maarufu NSSF ya zamani kuanzia saa moja usiku kwa kiingilio cha 10,000/=  wasiliana nasi kwa namba 0767831036. 

Mwenye kuhitaji kutuunga mkono katika kuendeleza tasnia ya Filamu Shinyanga na Tanzania tutakuletea tiketi yako popote ulipo. Tutaitazama Filamu hii mwanzo mwisho,siku hiyo ukumbi utageuka kuwa Jumba la sinema",amesema Songoro.

"Mimi Sio Mwehu ni filamu iliyosheheni misemo ya hekima itakayomfanya mtazamaji asichoke kuitazama katika maisha yake, washiriki wakuu kwenye filamu hii iliyoongozwa na Director Dave Skerah ni Juma Ibrahim Songoro, Goodness Mndeme na Fadhili Mungi",amesema.

Amesema Filamu hiyo imelenga  kuelimisha, kuonya na kuburudisha kwa kuangalia uhalisia wa maisha ya jamii zetu za Kiafrika.

Amewaomba mashabiki wa filamu kujiandaa kupokea Filmu hii yenye ubora wa hali ya juu.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527