BASI LA KIMOTCO KUTOKA ARUSHA KWENDA MUSOMA LAPATA AJALI



Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Kimotco kutoka Arusha kwenda Musoma mkoani Mara wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka eneo kati ya Itilima na Maswa mkoani Simiyu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, William Mkonda amesema ajali hiyo imetokea jana Alhamisi Septemba 5, 2019  saa 12 jioni.

"Hakuna vifo kuna majeruhi ambao bado hawajafahamika na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Maswa. Tunasubiri taarifa ya madaktari wa Maswa ili tutoe taarifa kwa umma,” amesema Kamanda huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527