MCHUNGAJI AFARIKI AKIFUNGA SIKU 30 ....SIKU ALIBAKIZA 10 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 6, 2019

MCHUNGAJI AFARIKI AKIFUNGA SIKU 30 ....SIKU ALIBAKIZA 10

  Malunde       Friday, September 6, 2019


Mchungaji Brighton Samajomba kutoka nchini Zambia, amefariki dunia kwa kinachotajwa kupatwa na Utapiamlo' akiwa katika mfungo ambao alikuwa anadhamiria kufikisha siku 30.

Mpaka anafariki mchungaji huyo alikuwa amefikisha siku 20 hivyo zilikuwa zimebaki siku 10 tu kutimia siku 30, Kaka wa Marehemu Reagan Samajomba anasema ndugu yake alikuwa na kawaida ya kufunga na kufanya maombi kwa muda mrefu kuliko wengine.

Katika mfungo wa siku 30 Kaka wa Marehemu anasimulia kuwa ndugu yake aliamua kufanya hivyo huku lengo kuu likiwa kuiombea familia yake pamoja na waumini wa kanisa analoliongoza mshikamano pamoja na umoja uzidi kuimarika.

"Jambo jema alilotuachia sisi kama familia ni namna alivyofariki sababu alikuwa karibu na Mungu," alisema Kaka wa Marehemu.

Vyanzo: Zambia watchdog, Nairaland, Iharare.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post