MOLINGA AWAKUNA MASHABIKI WA YANGA WAKICHAPWA 1 - 0 NA RUVU SHOOTING


Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa Yanga kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa timu hizo mbili.


Bao pekee na Ruvu Shooting limewekwa kimiani na Sadat Mohammed akimvisha kanzu kipa Farouk Shikalo mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza.

Bao hilo limeweza kudumu kwa dakika zote 90 mpaka Mwamuzi Martin Saanya alipohitimisha mchezo wa kupuliza kipyenga cha mwisho, ubao ukisomeka 1-0.

Katika mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera aliwatoa wachezaji Sadney Urikhob na kumwingiza Maybin Kalengo, Juma Balinya akimtoa pia na nafasi yake akichukua Balama Mapinduzi lakini mabadiliko hayakuleta mafanikio.

Ruvu imeweka rekodi kwa mara ya kwanza kufuta uteja kwa Yanga tena ikiibuka mshindi ikiwa ugenini.


Hata hivyo Mshambuliaji mpya wa Yanga, David Molinga amekonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza uwanja wa Uhuru kutokana na uwezo wake kupiga pasi za mwisho.

Molinga anacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu tangu alipotua Yanga, lakini ameshindwa kuisaidia timu hiyo kukubali kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Molinga alionekana kufanya vitu vya madaha kama kupiga visigino, pasi ya kifua na chenga ambazo ziliwainua mashabiki kwa kupiga shangwe la kushangilia.

Mashabiki hao hawakuishia hapo kumshangilia Molinga bali hata pale alipoonekana kupiga kichwa au shuti ambapo alionekana kukosa magoli ndani ya kipindi cha kwanza.

Molinga naye alionekana kuelewa shangwe hilo la mashabiki kuwa linamuhusu yeye kwani kuna wakati alionekana nae kuwainua mashabiki kwa kuwanyooshea mikono.

Mara baada ya mwamuzi Martin Saanya kupuliza kipyenga na kuamuru mapumziko kocha wa Yanga kabla ya kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo alionekana kumfuata Molinga na kuongea naye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527