WAZIRI MKUU MAJALIWA 'AKOSHWA' NA MAONESHO YA VIWANDA YA NCHI ZA SADC


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege nchini (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo kuhusu ya Reli ya Kisasa kutoka kwa Afisa Habari wa  Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania(TRC)  katika maonesho ya Wiki ya Viwanda SADC, yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa George Lous Chuwa kuhusu bidhaa mbalimbali wakati alipotembelea banda la Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

Na Mwandishi Wetu.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuchangamkia fursa zitokanazo na maonesho ya Viwanda ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wa viwanda ambao Serikali inaujenga.

 Akizungumza mara baada ya kutembelea maonesho hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja vya Karimjee na Gymkana, Waziri Mkuu amesema kuwa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC yamekamilika yakihusisha kuwepo kwa maonesho ambayo nchi wanachama wataonesha teknoloji, Ubunifu na bidhaa zao kutoka katika Viwanda vya nchi za SADC.

 Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imetoa fursa kwa wafanyabiashara Wakubwa, wa kati, wadogowadogo na wenye bidhaa zinazozalishwa kwa mikono kuja kuonesha na kuchukua teknolojia kutoka nchi wageni ambao wapo nchini kwa maonesho hayo ya wiki moja.

 “Sisi kama Serikali tumetoa Fursa kwa wale ambao wanafanya kazi na kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia mikono kuja kuonesha bidhaa zao ili ziweze kupata masoko kwa nchi wanachama wa SADC kwani nchi zote zinakuja hapa kuleta bidhaa mbalimbali kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii kuwauzia wageni bidhaa zetu”, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post