Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Kufanyika November 24,2019 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 23, 2019

Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Kufanyika November 24,2019

  Malunde       Friday, August 23, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 24, 2019.

Jafo ametangaza tarehe ya uchaguzi huo leo Ijumaa Agosti 23, 2019 wakati wa mkutano wake na wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wadau mbalimbali uliolenga kutoa maelekezo na tangazo la uchaguzi huo.Amesema kuwa tangazo hilo ni kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ibara ndogo ya 4,1 hadi 3 chini ya tangazo la serikali number 371  na kuendelea huku akisisitiza muhimu elimu ya mpiga kura  kutolewa  kwa wakati.


Amesema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi uandikishaji wapiga kura utaanza siku 47 kabla ya siku ya uchaguzi na utadumu kwa siku saba.

Amesema upigaji kura utaanza saa 2.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 12.00 jioni.

Waziri Jafo amesema viongozi watakoma uongozi wao  siku saba kabla ya siku ya  kuchukua fomu za kugombea.

Amesema waangalizi wa uchaguzi wataruhusiwa baada ya kupata kibali kutoka kwa katibu mkuu Tamisemi na maombi yatatakiwa  kupata kibali kwa katiba mkuu ndani ya siku 21 baada ya tangazo la uchaguzi kutoka.

Amesema kampeni sitafanyika siku saba kabla ya tarehe ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kutoa tangazo hilo katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi  Joseph Nyamuhanga amesema kanuni zote za uchaguzi zimekamilika  hadi sasa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wote wa mikoa nchini mkuu wa mkoa wa singida Dkt.Rehema Nchimbi amesema wako tayari katika maswala ya kiusalama,ulinzi na Amani sanjari na taarifa sahihi na za wakati kwa watu wote bila upendeleo na ubaguzi na utakuwa uchaguzi wa uhuru ,haki na uwazi. 
Wakizungumza mara baada ya tangazo hilo baadhi ya viongozi wa vyama tofauti wamesema kuwa huu ndiyo wakati muafaka wa kujipanga kwaajili ya uchaguzi huo. 
Ikumbukwe kila baada ya miaka mitano Tanzania bara  hufanya uchaguzi wa serikali za mitaa katika ngazi ya kata ,vijiji na mitaa kabala ya uchaguzi mkuu wa wabunge na rais miezi michache baadaye.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post